PPB - Services

Complaints, Feedback and Enquiry

HATI YA UTOAJI HUDUMA KWA MTEJA

[featured_image]
  • Version
  • Download 43
  • File Size 1.58 MB
  • File Count 1
  • Create Date January 15, 2025
  • Last Updated January 16, 2025

HATI YA UTOAJI HUDUMA KWA MTEJA

Halmashauri ya Kuthibiti Dawa na Sumu (Kama inavyorejelewa hapa kama 'Halmashauri') imetayarisha Hati ya Utoaji Huduma kwa Mteja kwa mujibu wa Kifungu 43 (1) (a) cha Katiba na kujitolea kwa serikali kwa wananchi wake kutoa kiwango cha juu iwezekanvyo cha utuzaji wa afya.

Mamlaka ya Halmashauri  ni kulinda na kukuza afya ya umma kwa kuthibiti taaluma ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa na vifaa vya matibabu bora, yenye kuleta matokeo yanayotakiwa na salama.

Halmashauri  inatambua kwamba hati ya huduma kwa mteja ni kiungo muhimu cha utoaji wa huduma kwa wakati na thabiti na ni mkakati muhimu wa kutimiza maono na malengo saidizi.    Zaidi, hati hii ya utoaji wa huduma kwa mteja ni mchakato jumla wa usimamizi utakaotumika katika ngazi zote za shughuli za taasisi.

Wadau na washirika wengine wanatambuliwa wakati wa utoaji wa huduma na kuhakikisha kuna usawa wenye heshima. Usimamizi, kila mara utatambua mahitaji ya mteja, kutathmini na kurekebisha hati ya huduma ili kuhakikisha kuna utoaji wa huduma wa kuridhisha.

Halmashauri  inatoa hakikisho kwa wateja na wadau wa kujitolea kwake kutimiza na kuzidisha matarajio yao. Utekelezaji wa Hati hii ya Utoaji Huduma kwa Mteja kwa hivyo kutaboresha utoaji wa huduma, uwajibikaji huku ikihakikisha mchango wake wa kulinda na kukuza afya ya umma.

Attached Files

FileAction
003_CEO_PQR_QMS_POL_HATI YA UTOAJI HUDUMA KWA MTEJA.pdfDownload

Author

Tony Kemboi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *